HUKMU YA KUMKUFURISHA MTU


Suali: Nataka kujua hukmu za kumkufurisha mtu.

Jawabu: Ama baada ya kumshukuru Mwenyezi Mungu na kumswalia Mtume Muhammad 
Haya ni Mas 'ala makubwa ambayo ndani yake nyayo zimeteleza na fahamu zimepotea , tunamuomba Mwenyezi Mungu alietukuka atuongoze katika njia ya haki kwa idhini yake hakika yeye ndie mwenye kumuongoza amtakae katika njia iliyo nyooka. Jua ALLAH akuwafikishe
Kwanza : Kumhukumia mtu ukafiri ni jambo la hatari kubwa, kwani kwa kumhukumia ukafiri damu yake inakua halali baada ya kua ilikua imezuiliwa, anasema Mtume MUHAMMAD S.A.W

 

أمرت أن أقاتل الناس حتى يقولوا لا إله إلا الله فمن قال لا إله إلا الله عصم مني دمه وماله إلا بحقه وحسابه على الله]    متفق عليه]

 

[Nimeamrishwa kuwapiga watu vita mpaka waseme Laa ilaha illa Allah Hapana mola apasae Kuabudiwa kwa Haki ila Mungu mmoja,basi atakae sema LA ILAHA ILLA ALLAH atapata himaya kwangu damu yake na mali yake isipokua kwa haki yake na hesabu yake iko kwa Mwenyezi Mungu]    [Imepokelewa na Bukhary na Muslim]

Na katika riwaya nyingine:

 

[حتى يشهدوا ألا إله إلا الله ويؤمنوا بي وبما جئت به]

 

[Mpaka washuhudie yakwamba hakuna mola apasae kuabudiwa kwa haki isipokua Mwenyezi Mungu na Waniamini mimi na niliyokuja nayo]

Na anasema Mtume:

 

أيما رجل قال لأخيه يا كافر فقد باء بها أحدهما]    متفق عليه]

 

[Mtu yeyote atakaemwambia ndugu yake ewe kafiri basi mmoja wao atabeba huo ukafiri]   [Imepokelewa na Bukhary na Muslim.]

Pili: Inathibiti sifa ya Uislamu kwa mtu baada ya yeye tu kukiri Uislamu, iwe kukiri huko ni kwa kutamka Shahada mbili au yanayochukua nafasi ya Shahada mbili ikiwa atashindwa kutamka Shahada mbili kutokana na kutoelewa Lugha ya Kiarabu au kwa kuto ongea yaani akawa ni bubu. Na lazima kutilia mkazo hakika moja muhimu nayo ni kwamba kusema yakwamba sifa ya uislamu inathibiti kwa mtu akitamka shahada mbili hilo halimaanishi yakwamba kukiri kwake huko hakuna mambo ambayo anatakiwa kujilazimisha nayo, kwani Ahlu Ssunna katika swala hili wako kati kati ya njia mbili zinazokinzana.

1. Njia ambayo watu wake wanaona yakwamba mtu kukiri Uislamu na kutamka Shahada mbili au kujidhihirisha na baadhi ya mambo ya Kiislamu haitoshi kumhukumu mtu kwamba ni Muislamu, bali ni lazima kubainisha wanaloliona kiwango cha chini cha Uislamu

2. Njia ambayo wanaona watu wake mtu kutamka Shahada mbili inatosha kuthibiti sifa ya Uislamu kwake na kubaki kwa sifa ile hata kama hatahakikisha yanayolazimiana na kukiri huko kwa kujilazimisha na matendo dhahiri.
Ama njia ya haki njia ya Ahlu Ssunna ni kutofautisha kati yanayolazimisha kuthibiti kwa sifa ya uislamu kwa mtu kwanza na baina yanayolazimisha kubaki kwa sifa hiyo na kuendelea kwa hukmu hiyo kwa mtu.
3. Ni lazima kutofautisha kati ya hukmu na kumuhukumia mtu, kwani sio kila mwenye kua na sifa Miongoni mwa sifa za kikafiri atakua Kafiri. Bali ni lazima kutofautisha baina ya hukmu juu ya kitendo kwamba ni ukafiri, na baina ya hukmu kwa mwenye kutenda kwamba ni kafiri, kutokana na tofauti inayohusiana na mambo haya mawili. Kwani hukumu juu ya kitendo cha dhahiri yakwamba ni ukafiri inahusiana na kubainisha hukmu ya kisheria moja kwa moja . Ama mtendaji basi ni lazima kuiangalia hali yake, kwa uwezekano wa kutokea sababu miongoni mwa sababu zinazozuia kumuhukumu ukafiri wake kutokana na ujinga au kulazimishwa au tofauti na hivyo, na hili linatokea kama itasimama hoja kwa mtu kwa kutokua na udhuru wa ujinga au kulazimishwa . na kusimamisha hoja haifanyiki isipokua kutoka kwa mwanachuoni.

Anasema Ibnu Taymiyyah (radhi za Allah ziwe juu yake)

"Haifai kwa mtu yeyote kumkufurisha yeyote katika waislamu hata akikosea na kuteleza mpaka asimamishiwe hoja na abainishiwe ukweli , na yule ambae Uislamu wake utathibiti kwa yakini basi hilo la Uislamu wake halitaondoka kwa shaka. Bali halitaondoka ila baada ya kusimamisha hoja na kuondoa utata" na akasema tena

"Hakika kukufurisha ina Masharti na vizuizi ambavyo vinaweza kukosekana kwa mtu, na ukufurishaji wa ujumla haulazimishi ukufurishaji wa mtu fulani mpaka masharti yapatikane na vizuizi vikosekane. Kisha akasema Ibnu Taymiyyah

"Alikua Imam Ahmad Mwenyezi Mungu amrehemu anawakufurisha kundi la JAHMIYYAH ambao walikua wanakanusha majina na sifa za Mwenyezi Mungu, kwa sababu ya kwenda kinyume maneno yao na aliyokuja nayo bwana Mtume Muhammad ﷺ na hili ni jambo la wazi ....... Lakini alikua hawakufurishi mmoja mmoja" yaani kusema mtu fulani ni kafiri

4. Ukafiri kama unavyokua kwa kuitakidi kwa moyo basi unakua kwa Maneno na Matendo pia. Anasema Ibnu Taymiyyah Mwenyezi Mungu amrehemu: "Ukafiri ni kutomuamini Mwenyezi Mungu na Mtume wake sawa ukafiri huo uandamane na kukadhibisha au usiandamane nao, bali mtu hukufuru kwa kutilia shaka na kupuuza kwa mambo yote haya kwa uhasidi au kiburi au kwa kufuata matamanio yanayomuepusha kufuata ujumbe wa Mitume".
Anasema Assubky: "Kukufurisha ni hukumu ya kisheria sababu yake ni kukanusha uungu wa Mwenyezi Mungu au umoja wake au utume wa Mtume au kauli au kitendo ambacho sheria imehukumu yakwamba ni ukafiri hata kama sio kukanusha".

Ukafiri unaweza kua kukadhibisha kwa moyo na ukafiri huu ni mchache kwa makafiri kama alivyosema Ibnul Qayyim, kwa sababu Mwenyezi Mungu aliyetukuka amewapa mitume wake miujiza na dalili za kuonyesha ukweli wao ambazo zimesimamisha hoja na kuondoa udhuru , na ukafiri unaweza kua kauli kupitia ulimi hata kama moyo unaswadikisha au hauitakidi huu ukafiri wa kauli . anasema Abu Thaur : "Na lau atasema : masihi (yesu) ndie mungu na akakanusha jambo la uislamu kisha akasema moyo wangu haujaitakidi jambo lolote katika hilo basi yeye ni kafiri kwa kudhihirisha hilo na wala sio muumini".
Anasema Mwenyezi Mungu alietukuka:

 

قُلْ أَبِاللَّهِ وَآيَاتِهِ وَرَسُولِهِ كُنتُمْ تَسْتَهْزِئُونَ لَا تَعْتَذِرُوا قَدْ كَفَرْتُم بَعْدَ إِيمَانِكُمْ ۚ}   التوبة:65-66}

 

[Sema: Mlikuwa mkimfanyia maskhara Mwenyezi Mungu na Ishara zake na Mtume wake?Msitoe udhuru; mmekwisha kufuru baada ya kuamini kwenu!]    [Tawba: 65-66]

Na anasema Ibnu Nujaym: Hakika mwenye kutamka maneno ya ukafiri kwa mzaha au kwa mchezo basi amekufuru kwa watu wote wala haizingatiwi itikadi yake . anasema Ibnu Taymiyyah : ukafiri unakua katika kumkadhibisha mtume kwa yale aliyoyaeleza au kukataa kumfwata na pamoja na kujua kwake ukweli wake kama ukafiri wa Fir'aun na mayahudi na wengineo . na anasema Ibnul Qayyim kuthibitisha yakwamba ukafiri unakua katika kauli matendo na itikadi pia : Na ukafiri una asili na matawi, kama vile matawi ya imani ni imani basi matawi ya ukafiri pia ni ukafiri na kuona haya ni fungu katika imani na upungufu wa haya ni fungu katika mafungu ya ukafiri. na anasema tena : Ukafiri ni aina mbili : ukafiri wa matendo na ukafiri wa kukanusha , na ukafiri wa kukanusha: Kwamba yeye anakufuru yale anayoyajua kwamba Mtume  ﷺ amekuja nayo kutoka kwa Mwenyezi Mungu - kwa kukanusha na ujauri - katika majina ya Mwenyezi Mungu na sifa zake na matendo yake na hukmu zake. Na ukafiri huu unaenda kinyume na Imani katika kila njia , ama ukafiri wa matendo unagawanyika katika makundi mawili ukafiri unaoenda kinyume na imani na ukafiri ambao hauendi kinyume na Imani , hivyo basi kusujudia sanamu na kuushusha hadhi mswahafu na kumuua Mtume na kumtukana inaenda kinyume na Imani) hivyo basi jua ewe Ndugu yangu Ttukufu Mwenyezi Mungu akupe tawfiq yakwamba Mas'ala haya ufafanuzi wake ni mrefu mno, haya ni machache tuliyojaaliwa , na huenda tumeleta suluhisho la jambo lililokusudiwa.

Na ALLAH ni mjuzi zaidi.


*Chanzo: Fatawa za Sheikh Al Munajid

Imefasiriwa na Mahamd Fadhil El Shiraziy


comments