NI YAPI MALIPO YA MZINIFU


 

Suali : Ni yapi Malipo ya Mzinifu ?

Jawabu : Ama baada ya kumshukuru Allah na kumswalia Mtume Muhammad ﷺ.
Zinaa ni harami na ni katika Madhambi akubwa baada Shirki na Kuua, Mwenyezi Mungu  anasema :

 

 

وَالَّذِينَ لَا يَدْعُونَ مَعَ اللَّهِ إِلَٰهًا آخَرَ وَلَا يَقْتُلُونَ النَّفْسَ الَّتِي حَرَّمَ اللَّهُ إِلَّا بِالْحَقِّ وَلَا يَزْنُونَ ۚ وَمَن يَفْعَلْ ذَٰلِكَ يَلْقَ أَثَامًا  يُضَاعَفْ لَهُ الْعَذَابُ يَوْمَ الْقِيَامَةِ وَيَخْلُدْ فِيهِ مُهَانًا إِلَّا مَن تَابَ وَآمَنَ وَعَمِلَ عَمَلًا صَالِحًا فَأُولَٰئِكَ يُبَدِّلُ اللَّهُ سَيِّئَاتِهِمْ حَسَنَاتٍ ۗ وَكَانَ اللَّهُ غَفُورًا رَّحِيمًا

 

[Na wale wasio mwomba mungu mwengine pamoja na Mwenyezi Mungu, wala hawaui nafsi aliyo iharimisha Mwenyezi Mungu isipo kuwa kwa haki, wala hawazini - na atakaye fanya hayo atapata madhara,Atazidishiwa adhabu Siku ya Kiyama, na atadumu humo kwa kufedheheka Isipo kuwa atakaye tubu, na akaamini, na akatenda vitendo vyema. Basi hao Mwenyezi Mungu atayabadilisha maovu yao yawe mema. Na Mwenyezi Mungu ni Mwenye kusamehe, Mwenye kurehemu.]    [Al Furqaan 68 - 70]

Na Mwenyezi Mungu anasema:

 

وَلَا تَقْرَبُوا الزِّنَا ۖ إِنَّهُ كَانَ فَاحِشَةً وَسَاءَ سَبِيلًا}    إسراء:32}

 

[Wala msikaribie uzinzi. Hakika huo ni uchafu na njia mbaya] [Al Israa 32]

Na amepokea Abdullahi bin Mas'uud radhi za Allah ziwe juu yake anasema:

 

سألت رسول الله صلى الله عليه وسلم: أي الذنب عند الله أكبر ؟ قال: [ أن تجعل لله نداً وهو خلقك ]. قلت : ثم أي ؟ قال: " أن تقتل ولدك خشية أن يطعم معك " قلت: ثم أي ؟ قال: [ أن تزاني بحليلة جارك ]    متفق عليه

 

Nilimuliza Mtume ﷺ ni dhambi gani kubwa mbele ya Mwenyezi Mungu ? Akasema : [Ni kumfanyia Mwenyezi Mungu mshirika yeye ndie aliyekuumba] nikasema : kisha ni Dhambi gani tena ? Akasema : [Ni kumuua mwanao kwa kuhofia asile na wewe] nikasema : gani tena ? Akasema : [ni kuzini na mke wa jirani yako ]    [imepokelewa na Bukhary na Muslim.]

Na wamekubaliana watu wa mila zote kuhusu uharamu wa zinaa.

Na inatofautiana dhambi ya zinaa na ukubwa wake kulingana na vyanzo vyake , kwani kuzini na Mahaarim (yaani wanawake ambao mtu hafai kuwaoa) au kuzini na mwanamke alieolewa dhambi yake ni kubwa kuliko kuzini na mwanamke wa nje au mwanamke ambae hana mume , kwani katika kuzini na Mke wa mtu kuna kuvunja heshima ya Mume na ni kuharibu kitanda chake na kumuunganishia nasaba ambayo sio yake , na yasiokua haya katika maudhi , Allah atuokoe na na yanayosababisha hasira zake.

Ama Adhabu ya mwenye kuzini : Ikiwa mwenye kuzini yupo huru na ameoa au ameolewa atapigwa mawe hadi kufa awe mwanamume au mwanamke, na hili ni jambo Wamekubaliana nalo Wanazuoni na wamejumuika katika hili. Anasema Ibnu Qudamah: "Na wamekubaliana kuhusu jambo hili Maswahaba wa Mtume ﷺ, na imepokelewa kutoka kwa Imam Ahmad riwaya yakwamba mwenye kuzini na ameoa au kuolewa atapigwa mijeledi kisha atapigwa mawe, na dhehebu la wanazuoni ni kwamba adhabu ni kupigwa mawe tu", hivyo hivyo wamekubaliana Wanazuoni wa Fiqhi yakwamba mwenye kuzini na hajaoa Mwanamume au Mwanamke atapigwa Mijeledi mia moja akiwa huru, ama Mtumwa na kijakazi adhabu yao ni mijeledi hamsini sawa wawe mabikira au wameshaoa kwa Neno lake Mwenyezi Mungu:

 

فَإِذَا أُحْصِنَّ فَإِنْ أَتَيْنَ بِفَاحِشَةٍ فَعَلَيْهِنَّ نِصْفُ مَا عَلَى الْمُحْصَنَاتِ مِنَ الْعَذَابِ}   النساء:25}

 

[Na wanapo olewa kisha wakafanya uchafu basi adhabu yao itakuwa ni nusu ya adhabu waliyo wekewa waungwana.]       [An Nissai:25]

Kisha ikiwa aliezini ni bikra na yuko huru , basi madhehebu ya imam shafii na imam Ahmad bin hambal wamewajibisha kumfukuza huyu aliezini mwaka mzima kutoka mahali alipozini sawa awe Mwanamume au Mwanamke, na Madhehebu ya Imam Malik yamewafikiana na madhehebu mawili yaliyotangulia katika kufukuzwa Mwanamume peke yake na sio Mwanamke , na huenda kauli sahihi ni ile ya kwanza kwamba wanafukuzwa wote Mwanamume na Mwanamke.Kwa Hadithi ya Mtume :

 

[خذوا عني خذوا عني قد جعل الله لهن سبيلاً : البكر بالبكر جلد مائة ونفي سنة ، والثيب بالثيب جلد مائة والرجم]

 

[Chukueni kutoka kwangu chukueni kutoka kwangu Mwenyezi Mungu ashawatolea njia Wanawake watakaozini : bikra kwa bikra watapigwa Mijeledi Mia moja na watafukuzwa Mwaka mmoja, na alieoa kwa alieolewa watapigwa mijeledi mia moja na Mawe]

Katika hadithi hii Mtume hakutofautisha kati bikra Mwanamume au Mwanamke katika kufukuzwa Hadithi ameipokea na Imam Muslim katika Sahihi yake katika hadithi iliyopokelewa na Ubadah bin Swamit radhi za Allah ziwe juu yake.

Na Allah ni mjuzi zaidi.


*Chanzo: Fatawa za Sheikh Al Munajid

Imefasiriwa na Mahamd Fadhil El Shiraziy


comments