JE INAFAA KWA MWANAMKE KUKIHAMA KITANDA CHA MUMEWE IKIWA MUME UKO NA UGONJWA?
Suali: Je inafaa kwa Mwanamke kukihama kitanda cha mumewe ikiwa Mume uko na ugonjwa?
Jawabu: Niwajibu kwa mwanamke kumtii mumewe na kumtekelezea haja zake zote anazo hitajia, ikiwemo haki ya kulala nayeye, na haifai kwa mwanamke kukihama kitanda cha mumewe asipokuwa na udhuru wa kisheria,amepokea Abuu Hurayrah radhi za Allah ziwe juu yake kutoka kwa Mtume ﷺ amesema:
إذا دعا الرجل امرأته إلى فراشه فأبت أن تجيء لعنتها الملائكة حتى تصبح.] متفق عليه]
[Mume atakapo mwita mkewe katika kitanda chake,(mwanamke) akakataa kumjilia, basi hulaniwa na Malaika mpaka ipamzuke] [Imepokelewa na Bukharin a Muslim]
Lakini ikiwa mwanamume amepatikana na ugonjwa wakuambukiza,na mke akakhofia kuambukizwa na ugonjwa ule,au akawa mume anajambo la kukirihisha lisilo wezekana kwa mtu kustahimili, basi anapo kataa kumuitikie mumewe hahisabiwi kuwa ameasi,na kwa hali hii mwanamke anakuwa na khiyari baina ya kutaka talaka, au kumsubiria mumewe,ama ikiwa ugonjwa si wakuambukiza wala siudhia ambao hausthimiliki basi mwanamke anakuwa hana udhuru wakukata kumuitikia mumewe anapo mtaka kulala na yeye ,na akikataa huhisabiwa kuwa ameasi, na mume atakuwa na haki kumyima haki zake nyingine kama chakula na mavazi na malazi na mengineo.
Na Allah ndie mjuzi Zaidi.