Menu

AR-RAHEEQ AL-MAKHTUM


Quresh


Baada ya uchunguzi inaonekana kuwa japokuwa mpaka wakati huo Da'awa ilikuwa bado ni ya siri, Makuraishi walikuwa wamekwisha kusikia khabari za Mtume na mafundisho yake, lakini wao walizipuuza khabari hizo. 

Muharnmad Al-Ghazali amesema, "Khabari hizi zilienea kwa Makuraishi, lakini wao hawakuzipa umuhimu wowote, na huenda walimdhani kuwa Muhammad ni mmoja wa hao watu ambao wanajihusisha na masuala ya dini, wanaozungumzia mambo ya Uungu na haki zake, kama alivyofanya Umayya bin Abi As-Salti na Quss bin Sa'idah, , Amru bin Nufail, na wengineo. Makuraishi walizinduka baada ya kipindi fulani kupita, walianza kupata khofu kwa jinsi ujumbe wake ulivyoenea kwa kasi na jinsi watu walivyokuwa wakiupokea na kuenea kwa athari yake, wakaanza kufuatilia safari zake na Da'wa yake kwa makini zaidi." (1)

Wito wa siri uliendelea kwa muda wa miaka mitatu, na katika kipindi hiki, liliibuka kundi la Waislamu ambalo lilisisitiza udugu na ushirikiano, kuueneza ujumbe na kumtia hima Mtume katika msimarno wake. Baada ya hapo ndio sasa ukashuka Wahyi uliomtaka Mjumbe wa Mwenyezi Mungu kuwatangazia Dini watu wake kwa kuwabainishia haki na batili pamoja na kuyahujumu rnasanarnu yao. *


1) Fiqlti Sira, Uk. 76.

* Ar Raheeq Al Makhtuum 123


 

LOGOISLAM

Search Videos

RSS Content

<

 

WhatsApp This Page Now
 

Visitors Counter

6575414
TodayToday121
Highest 01-07-2025 : 4073
US
Guests 9

Mkurugenzi na naibu wake

SS10

 

VIKAO VYA OFISI

title_6829791e8c7562696728241747548446
title_6829791e8c84116258189931747548446
title_6829791e8c92712981560771747548446

NISHATI ZA OFISI

title_6829791e8df3814304996371747548446
title_6829791e8e01c5256385551747548446
title_6829791e8e0fe2503468501747548446 Add content here

HUDUMA MPYA

: 9 + 15 =

IslamChoice- Kiswahili

Ni mtandao mpya wa ulinganizi unao funza mafunzo ya dini ya kiislamu kuambatana na Qur'ani na Sunna za Bwana Mtumeﷺ zilizo sahihi‎ kwa ufahamu wa wema walio tutangulia.

UongofuUongofu.com