KUSILIMU KWA MYAHOODI RABII YOUSEF COHEN
Rabii Yousef Cohen alizaliwa Brooklyn, Amerika mwaka wa 1971, alikuwa mfuasi wa satmar, kikundi katika makundi ya kiyahoodi akiitwa Joseph Cohen. Alioa Lona Cohen myahood kama yeye na wakajaaliwa watoto wane.
Mwaka wa 1998, alisafiri Israeli na kuishi katika makaazi ya Ghosh Gatif, katika ukanda wa Gaza na baadaye akaghura kwenda Netivot kusini mwa Israeli. Rabii Yousef Cohen alikutan na Waislam kwa mara ya kwanza katika safari yake ya mara kwa mara katika soko la zamani huko Jerusalem, na akapewa kwa mara ya kwanza tafsir ya Quraan kwa lugha ya kiingereza.
Katika mahojiano na channel 10 TV alisema,
Nilipofunguwa Quran [tafsir] kwa mara ya kwanza, sikuweza kuiweka chini. Nikile nilikuwa
Naamini vile uyahoodi unatakiwa uwe. Kila kukosolewa kwa wayahood katika Quraan kulikuwa
Sawa na bila chuki. Bila shaka Allah akituonyesha wayahood, namna ya kujirudi wenyewe na
Kuirudia Haki [Uislam] ya Mwenyezi Mungu’
Baada ya utafiti wake, Rabii Yousef Cohen alimkabili mkewe Lona Cohen, mfuasi sugu wa uyahoodi akisema, nakupenda, na nataka kuwa mkweli kwako……… nimesoma Quraan, na nakubaliana na yote yaliyoko ndani yake, na nikiendelea mimi nina dini ya uyahoodi ntakuwa si mkweli’.
Baada ya mazungumzo hayo na mkewe, alisilimu na kupewa jina, Yousef Mohammad al Khattab, mkewe alishtuka mno, naye akaanza kutafiti kwa msaada wa mumewe,na baada ya majuma matatu, Lona Cohen pamoja na wanawe wanne wakasilimu na kuiacha dini ya uyahood.
Muda mchache walihama hadi Al-Toor magharibi mwa Jerusalem wanako ishi hata leo. Al-Khattab anafanya kazi katika shirika la Kiislam, na mno anawalingania wayahoodi waje katika Uislam. Kitendo hichi cha kuwalingania wayahoodi Uislam kimemfanya achukiwe sana katika Israeli na kupendwa san asana na jamii ya Waislam.
Angalia kitabu
They are extremely smart or
Extremely ignorant
HISTORIA YA MAMA AMINAH ASSILMI
Waliosilimu wanazo changamoto nyingi na zinazotishia, hivi kwamba asiye na imani kamili aweza kuteteleka na kurudi nyuma. Lakini wale waliojaaliwa na Allah [swt] husimama kidete na historia zao twazisoma hata leo, nakila zikisomwa sisi hupata mafunzo ya subira katika yanayotusibu kama vile Sahaba mtukufu na Muadhin wa Mtume [saw], Seyyidna Bilal [ra], kadiri mateso yalivyozidi alikisema ‘Ahad, Ahad,Ahad’.
Katika miaka yetu hii tunao watu walioonyesha misimamo imara licha a mateso waliokuwa wakipitia, mfano ni mama Aminah Asilmi aliyezaliwa Oklahoma, Amerika na kubatizwa katika kanisa la Southern Baptist. Alifuzu katika chuo na shahada ya uanahabari, haswa utangazaji wa TV, na akajitokeza kama mtetezi wa haki za wanawake, aliupinga Uislam eti unawanyanyasa wanawake, alitaka uhuru wa mavazi, pamoja na kuhoji kwa nini katika Uislam wanawake hawaruhusiwi kuolewa na mume zaidi ya mmoja hali waume wameruhusiwa kuoa mke zaidi ya mmoja.
Historia ya kusilimu kwake inaanza pale kosa la kitarakilishi, akasajiliwa katika kitengo cha michezo ya kuigiza ya TV, japo kuwa mwenyewe hakutaka kuingia katika kitengo hicho, lakini uwepo wa wanafunzi wenzake watatu Waislam, naye akiwa mkereketwa wa ukristu akaona abakie katika kitengo hicho ili awakaribishe hao Waislamu katika ukristu. Alitumia mbinu ya zamani ya wakristu eti ‘ Yesu anawapenda Waislam na alikufa kwa ajili ya kuwaokoa na dhambi zao’
Mwenyewe aliona ajabu kuwa alitaka kuwatoa Waislamu katika Dini yao, lakini mwishowe akawa ni mwenye kusilimu!, Baada ya kukumbana na Waislam kwa mara ya kwanza, alianza kutafiti kwa miaka miwili lengo ni yeye apate wepesi wa kuwaleta waislamu kwa ukristu. Katika kipindi hichi aliisoma Quraan tafsiri yote na hoja alizozipata alikubaliana kabisa na Imani na Dini ya Kiislamu, na akaamua kusilimu kwa khiari yake tarehe 21/5/1977, akaanza kuvaa mavazi ya sitara pamoja na kufuata yote aliyokuwa akipinga.
Tendo hili la Kusilimu kwake lilimfanya apoteze marafiki wake aliokuwa akishirikiana nao katika pati za kila weekend maana hakushiriki tena katika maasi yao. Dada yake aliyekuwa mtaalam wa akili alimuona kama aliyepoteza akili, naye Baba mzazi aliposikia binti yake amesilimu aliazimu kumwua kwa risasi, kwa kuwa aliona afadhali ‘awe amekufa’. Mumewe, baba wa watoto wake wawili naye alimpa talaka, na kazini akatimuliwa eti kuvaa baadhi ya nguo kutawatishia watazamaji.
Alipo enda mahakamani ili adai haki yake ya kukaa na kuishi na wanawe, alinyimwa haki hiyo na jaji alimwambia achague baina ya mambo haya mawili:
1. Aukatae Uislamu apewe watoto au
2. Abakie Muislam na awasahau watoto.
Hebu fikiri kumzuia mzazi wa kike asiwakaribie watoto wake au kuwaona!, huku nyuma wakristo wakawa wanadai kuwa ni adhabu kwa kuuasi Ukristu, kwa hivyo watoto wakakabidhiwa mtalaka wake, alibakia na majonzi lakini akafanya subira ya hali ya juu. Alibakia na Uislamu wake na kuendelea kuwa mzuri kwa jamaa zake akiwaonyesha heshima ya Uislam, akajiepusha na matendo yote maovu, na ajabu Allah [swt] , wale walio kuwa maadui wakaanza kumkaribia, na wakwanza kuukubali Uislam ni nyanya yake mwenye umri wa miaka zaidi ya mia moja [100], kisha baadaye baba yake aliyetaka kumwua kwa kusilimu, kisha mama yake, dada yake aliyemuona kuwa wazimu kwa kusilimu kwake, mtalaka wake pia alisilimu na watoto wakasilimu walipo fikia umri wa miaka ishirini na moja [21]. Angalia neema ya Uislam!.
Aminah Asilmi hakumrudia mtalaka wake, bali aliolewa kisheria na mume mwingine na Allah akamjaalia mtoto wa kiume. Twaweza kusema kila alichopoteza hapo mwanzo, Allah [swt] alimrudishia na kumpa kazi kubwa na ni ulinganizi kupitia shirika la International Union of Muslim Women.
UISLAMU NI DINI YA MANABII WOTE
Sifa zote njema ni zake Allah,Muumba wa mbingu na ardhi,Muumba wa vinavyoonekana na visivyoonekana, Allah ambaye amemtuma Mtume ﷺ kwa uongofu na kwa Dini ya Haki ili ajaaliye ishinde dini zote japo kuwa watachukia makafiri. Rehma na amani zimwendee Mume ﷺ, na Familia yake Tukufu,maswahaba wake watukufu, na wote waliomfuata hadi siku ya malipo Ameen.
Tunamshukuru Allah [swt] aliye tuumba sisi kuwa wanadamu,wala sio wanyama, na akatujaalia akili ili tuchanganue mema tuyafuate, na mabaya tuyaepuke, na juu ya yote Tunamshukuru Allah [swt] aliye tujaalia sisi kuwa Waislam wanaomwabudu pasina kumshirikisha na viumbe vyake au madai yasiyo ingia akilini.vile vile tunamshukuru Allah[swt] kuwa katika ummati Muhammad ﷺ.
Uislam ni Dini iliyokamilika kwa Nyanja zote , na ni mfumo kamili wa maisha. Uislam umejengwa kwa nguzo tano muhimu, shahada,sala,saumu,zakaa na hijja na vyote hivi vyalingania vitu viwili, Umoja na Tabia nzuri katika mazungumzo,ibaada, mavazi n.k, jambo ambalo ni muhali kwa madini yaliyosalia.
Ndugu msomaji,sisi waislam twawafundisha ndugu wakristu kwa Heshima ya Uislam,sio kwa dharau zao,tunakupa ukweli wa Quraan wala siyo propaganda ya vitabu vyao,tunakupeni maandiko kwa haki na usahihi, wala siyo chuki inayobainika kwa midomo yao. Mara nyingi wao huongeza au kupunguza maneno ya Allah [swt] ili kutafuta faida za kidunia [Quraan 2:79], sisi twakutakieni paradise na insha Allah ujumbe utakufikieni.
Kila tunapokuwa katika kutoa darsa,mahubiri au mafundisho, lazima kutoa ushahidi, ni lazima uwe mkweli kwa nafsi yako kwanza unapo soma Maandiko Matukufu, wazungu wanasema, "If quoting Maintain Accuracy, If Claiming Provide Proof " na mara nyingi wengi katika ndugu wakristu hawazingatii misingii hii muhimu ya mazungumzo! Mazungumzo ni njia ya kupeana fikra , na lazima upendo udhihirike, lakini kwa kumtukana Allah [swt], Mtume ﷺ pamoja na Waislam, sidhani kama kuna chochote kinachoweza kutuvutia.
Napenda ndugu wakristu wajuewazi kuwa Uislam ni Imani kuwa Mola ni Mmoja tu,na ndiye aliyeweka njia na mikakati maalum ya Ibaada na Maombi ambayo haikubali kamwe mifano au masanamu kwa namna yoyote. Katika Uislam Allah [swt] pekee ana uhai wa milele, na chochote kinachofikwa na al-maut hakiwezi wala hakifai kuabudiwa kwa namna yoyote ile, kwa hivyo uhusiano baina ya kiumbe na Muumba ni wa moja kwa moja wala hatuhitaji washenga kama walivyo ndugu wakristo, na Manabii wote ni waonyaji, viongozi na Mitume na wao pia walifanya Ibaada kwa Allah[swt] tena kwa bidii kubwa, na ndio ile Dua maarufu ya Rabbana aatina fiidunia hasana, wafil akheerati hasana ……………. .
Uislamu unakubali kuwa Muislamu aweza kushawishiwa na nafsi yake na akafanya uovu dhidi ya Allah [swt],au kuwakosea wanadamu wenzake, na kwa hili kila mmoja atachukua mzigo wake mwenyewe, wala hatuwezi kusema eti hayo ndiyo maamrisho ya Uislamu, kwa hivyo propaganda za wamagharibi,dola zetu na wakristu hazina athari kwa Uislamu na ndio sababu wamagharibi wengi wanaingia kwa Uislamu MAKUNDI MAKUNDI. Ndugu msomaji lengo la Uislamu ni kutoa mfumo kamili wa maisha bila kuacha sehemu yoyote ya maisha ya kiumbe huyu mwanadamu, naleo ndiye hasimu mkuu wa Allah [swt]
NA katika sehemu hii tutamulika wale watu mash'huri ulimwenguni waliopata nuru ya Uislamu na wakasilimu na kuweza Kuathiri wafuasi wao na wao kuwa waislamu.
MUHAMAD ALI CLAY
Katika watu Mash'huri walio ongoka na kupata Nuru ya Uislamu ni Muhamad ali
Muhammad Ali alizaliwa mwaka 1942 katika mji wa Louisville, Kentucky, kwa familia maskini ya Wamarekani weusi mnamo 17 Januari 1942 akijulikana kwa jina la Cassius Marcellus Clay
Alipata usumbufu yeye na familia yake kutoka ubaguzi wa rangi ambayo ilikuwepo katika
kipindi hicho.
Alikuwa mwanamasumbwi mstaafu kutoka nchini Marekani. Amepata kuwa bingwa wa uzito wa juu mara tatu.
Alisilimu mwaka 1975 na baada ya kusilimu na kujua dini ya haki alikwa na msimamo imara katika dini jambo lililo mpelekea kuhukumiwa badda ya kukataa kushiriki katika vita Vietnam mwaka 1967.
Alikamatwa na kupatikana na hatia juu ya rasimu ya ukwepaji mashtaka, wakamvua taji lake la uwanamasumbwi, na leseni yake ya uwanamasumbwi ikazuiliwa. Hakufungwa, lakini hakupambana kwa takriban miaka minne mpaka hapo rufaa yake ilipofanyiwa kazi na Mahakama Kuu ya Marekani, ambapo akaja kushinda.
Na alijulikana baada ya kusilimu kwake kuwa mtu mtulivu na kulingania amani duniani.
Hakuwa ni mwenye kujiona au kijangamba bali alikuwa akiona watu wote ni sawa mbele ya Mwenyezi Mungu.
Na mwaka 1972 alifunga safari ya kwenda Makkah kuhiji,na baade kuzuru sehemu kadha katika nchi ya Saudia na kulakiwa na wanachi na wakuu wa nchi hiyo.
Na baada ya kustafu katika mchezo wa ndondi alijihusisha katika kufanya matendo ya kusaidia wasio jiweza ,nchini America na sehemu mbali mbali duniani.na alipewa zawadi na umoja wa mataifa kwa juhudi yake katika kusaidia watu.
Na alichangia kujenga misikiti zaidi 170 nchini America na kusilimisha watu wengi.
Na walipotaka Hollywood kuwakirimu wasanii mbali mbali katika Los Angeles Januari ya mwaka 2002 alikataa kuwekwa nyota yake kwenye sakafu na watu kutembea juu yake kwa sababu ya kuhishimu jina la mtume Muhammad licha ya kuweko zaidi ya wasini 2500 ni mwana sanii peke jina lake limeandikwa kwenye ukuta wala halikuandikwa kwenye sakafu ya watu kutembelea.
Na kwa matokeo wa mchezo wa ndondi alipawa na Ugonjwa wa Parkinson 1984 na alikuwa ni mwnye subira na alikuwa akisema Allah amenioja ili kumjulisha kuwa simkubwa bali yeye allah ndie mkubwa
Na tarehe 2/6/2016 alilazwa Phoenix Hospital katika wilaya ya Arizona baada ya kuzidiwa na maradhi na terehe 4/6/2016 alifariki Dunia akiwa na umri wa miaka 74.
Na kuzikwa katika mji wake aliozaliwa Jiji la Louisville.
Mungu amuweke pema pamoja na wema.
Ni mtandao mpya wa ulinganizi unao funza mafunzo ya dini ya kiislamu kuambatana na Qur'ani na Sunna za Bwana Mtumeﷺ zilizo sahihi kwa ufahamu wa wema walio tutangulia.